Friday, August 19, 2016

MALKIA WA TAARABU SHAKILA SAIDI AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. 
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. Addo November, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa  alikutwa amekwishafariki. Taarifa kamili  ya mipango ya mazishi 
tutawaletea mara tu tutapozipata.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA
Post a Comment