Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kabla ya hafla fupi ya kusherekea miaka 19 ya benki hiyo na kuzindua wa huduma tatu za benki hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha hatari wa Benki ya Exim David Lusala. kulia ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
Mkuu wa kitengo cha hatari wa Benki ya Exim David Lusala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards) ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA. Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii. jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
Mkuu wa kitengo cha hatari wa Benki ya Exim David Lusala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha uhasibu, George Binde.
Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akikata utepe kuzindua huduma ya Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akionesha bango la huduma ya Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwasha mishumaa kwenye keki kusherekea miaka 19 ya benki hiyo hapa nchini jijini Dar es Salaam.
BENKI ya Exim Tanzania imesheherekea kuadhimisha miaka 19 ya ukuaji na uvumbuzi kwa kuzindua huduma mpya tatu kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda amesema kuwa leo wanasherekea miaka 19 tangu kuwepo hapa nchini ikiwa na mafanikio makubwa Katika miaka 19, benki hiyo imejenga utendaji bora na imara katika fedha wakiwa na rasilimali zenye thamani ya TZS 1.5 Trilioni kufikia Juni 2016.
Amesema kuwa Faida kabla ya kodi katika kipindi cha pili cha mwaka ilikuwa shilingi bilioni 64 na pia wameweza kuwa na wastani wa ukuaji kwa mwaka wa asilimia 30.
Mafanikio ya benki ya Exim Tanzania ni kuweza kuwa na makao nchini Uganda kwa kununua benki ya Imperial ya Uganda mapema mwaka huu. Benki ya Exim sasa ina hisa za asilimia 58.60 katika taasisi hiyo mpya ambayo inayofanya biashara kama Benki ya Exim Uganda. Wakati ikijikita kuwa benki ya kikanda tayari ina matawi 43 katika nchi nne zikiwemo Tanzania, Uganda, Djibouti na Comoro na pia ikiwa na mipango ya kuendelea kujitanua katika masoko mengine katika miaka mitano ijayo.
Amesema kuwa huduma zilizozinduliwa ni:-
1. Uwezo wa kutoa taarifa za udanganyifu katika kampeni ya kupambana na udanganyifu ikiwa na lengo la kutengeneza mazingira ya kutokuwa na wizi katika tasnia ya benki.
2. Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards) ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA. Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii.
3. Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa.
Katika miongo miwili iliyopita, ukuaji wa benki hii na mchango wake wa kiuc humi na kijamii umetambulika sio tu katika Tanzania bali pia katika kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa sababu ya ubora katika utendaji wake.
Comments