Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka barani Ulaya leo Jijini Dar es salaam, kulia ni Meneja Uendeshaji Ronald Baraka Shelukindo na kushoto ni Afisa Masoko Furaha Samalu.
Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande akimkabidhi mwandishi wa habari wa Kituo cha TBC Evance Mhando dekoda ya DSTV leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa michezo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande jijini Dar es Salaam leo.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia kisimbuzi cha DSTV kimezindua msimu mpya wa soka barani Ulaya huku kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza ikitangazwa kwa lugha ya kiswahili. Msimu huo mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 13 unat anatarajiwa kuwa wa kipekee hasa baada ya kupunguza bei kwa watumiaji wapya ambapo watapata kwa dekoda kwa shilingi 79,000.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwaka mpya wa Soka, Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande amesema kuwa msimu huu mpya utakuwa ni wa kipekee sana kwani kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza itakuwa inatangazwa kwa kiswahili ambapo watanzania wataweza kuelewa vizuri sana na hii itakuwa ni muendelezo kama ilivyo ligi ya Hispania.
Chande amesema kuwa watu mwaka huu watapata na nafasi ya kuangalia burudani ya mpira na takribani mechi 300 zitakazonyeshwa moja kwa moja ambapo SuperSport wataonyesha kupifia chaneli za SS3, SS5, SS6, SS7 na SS11 kwa ligi kuu ya Uingereza huku ligi ya Hispania ikiwa ikionyeshwa kupitia kifurushi cha DSTV Compact.
Meneja Mauzo wa Multichoice, Baraka Shelukindo amesema kuwa mbali na kupungua kwa bei hiyo, channeli zimeingizwa katika kifurushi cha 84,000 na pia kwa sasa wapo kwenye mikakati ya kuandaa application mpya ya ya SuperSport ambazo zitakuwa na live Streaming pamoja na video zilizojiri za kuvutia.
Katika uzinduzi huo DSTV walichezesha droo na kuwapatia dekoda waandishi wanne wa habari.
Comments