EFM KUZINDUA TAMASHA LA MUZIKI MNENE AGOSTI 28 MWAKA HUU KATIKA ENEO LA BOKO JIJINI DAR

 Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo akizungumza leo na waandishi wa habari (hapo pichani) juu ya tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama muziki mnene ambalo litaanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko  jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom, Nandi Mwiyombella akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

REDIO ya burudani ya Efm imezindua tamasha la kila mwaka lijulikanalo kwa jina la MUZIKI MNENE,ambalo linatarajia kuanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo amesema tamasha hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki 12 sawa na miezi mitatu ambapo muziki utapigwa  katika bar 12 za vijijini vya Dar es Salaam na  Pwani ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Tunasepa na kijiji '.

Alisema mziki mnene mwaka huu itaenda sambamba na kampeni ya nje ndani ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku nne mfululizo.

Ssebo alivitaja vipindi hivyo kuwa ni Uhondo ambacho kitafanyika siku ya jumatano, Sports headquarters siku ya Alhamisi, joto la asubuhi siku ya Ijumaa na Funga mtaa siku ya jumamosi ,ambapo pia utapigwa muziki wenye ladha ya singeli kwa lengo la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki huo.

Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano vodacom Nandi Mwiyombella alisema wanafurahi kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon."Burudani ndio sehemu ya maisha ya kila mtu na lengo ni kuhakikisha kwamba wateja wetu anapata burudani ya muziki kupitia Efm,"amesema Nandi.

Comments