RC MASENZA AWAFARIJI YATIMA WA KITUO CHA FARAJA MGONGO KWA MISAADA YA MILIONI 7.2.

Wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati yaliyotolewa msaada na RC Iringa .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akimkabidhi msaada wa bati 100 pamoja na madawati 100 vyote vikiwa na thamani ya Tsh milioni 7.2 mkuu wa kituo cha Yatima cha Faraja Mgongo kata ya Nduli Manispaa ya Iringa Padri Franco Soloberi jana , mkuu huyo ametoa msaada huo kufuatia janga la moto lililoteketeza majengo ya kituo hicho mwezi uliopitaanayeshuhudia kushoto ni diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
Diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtoveakimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kutekeleza ahadi yake ya madawati na bati.
Viongozi na watoto wanaolelewa kituo cha Faraja Mgogo wakimsikiliza diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
 Viongozi na watoto wanaolelewa kituo cha Faraja Mgogo wakimsikiliza diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
RC Iringa Amina Masenza akimkabidhi mkuu wa kituo cha yatima cha Faraja Mgogo Padri Franco Soloberi madawati 100 kulia ni diwani wa Nduli Bashir Mtove 
Diwani wa Nduli Bashir Mtove na mkuu wa kituo cha Faraja Padri Franco wakipiga makofi kumshukuru RC Masenza kwa msaada wake.
Jengo lililoungua.
Watoto yatima wakimpongeza RC Masenza kwa msaada wake.
Bati 100 zilizotolewa na RC Masenza.
 Madawati 100 yaliyotolewa na RC Masenza .
RC Masenza akionyeshwa ramani mpya iliyochorwa na Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kituo hicho.
Na MatukiodaimaBlog 
MKUU wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amekabidhi msaada wa madawati 100 na bati 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 7.2 kwa kituo cha kulea yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Faraja Mgongo baada ya kituo hicho kuteketea kwa moto mwezi mmoja uliopita .

Akikabidhi msaada huo leo kituoni hapo mkuu huyo wa mkoa aliyeongozana na kamati yake ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa alisema kuwa mara baada ya kituo hicho kuungua moto alifika kituoni hapo na kati ya ahadi alizopata kutoa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo hicho pamoja na madawati kwa ajili ya wanafunzi hao ahadi ambayo ameitimiza kwa wakati.

Bi Masenza alisema kuwa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dr John Magufuli ni serikali ya kuwatumikia wananchi hivyo akiwa ni mwakilishi wa Rais ngazi ya mkoa ataendelea kuwatumikia wananchi na kuona hakuna mwanafunzi anayekaa chini na ndio sababu ya kutoa madawati hayo 100 ili kuwawezesha wanafunzi hao kusoma vizuri.

“ mkoa wa Iringa umejipanga vizuri kuwatumikia wananchi wake na ndio maana baada ya moto huu kuteketeza jengo la watoto hawa yatima nimekuwa bega kwa bega na uongozi wa kituo ili kuona jengo hilo linajengwa kwa wakati “

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema aliagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuchora ramani mpya ambayo tayari ili majengo hayo yajengwe kwa ustadi kama njia ya kuepusha madhara makubwa kwa watoto pindi moto unapotokea .

“ Tunamshukuru Mungu wakati moto unatokea katika jengo hili watoto wote hawakuwepo ndani walikuwa nje ya kituo hicho kwa ziara ya mafunzo ila kama wangekuwepo ndani jinsi majengo hayo yalivyojengwa yawezekana yangetokea madhara mengine kwa watoto …..ramani hii mpya itasaidia majengo hayo kujengwa kwa kuzingatia majanga pindi yanapojitokeza kwa watoto kutoka kirahisi zaidi”

Diwani wa kata ya Nduli Bw Bashir Mtove pamoja na kumpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kuwasaidia watoto hao waliopo kata yake bado alisema bado msaada zaidi unahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho .

Alisema watoto hao bado wanakabiliwa na mahitaji mbali mbali yakiwemo ya mavazi na vifaa vya masomo ambavyo vyote viliteketea kwa moto huo .

Bw Mtove alisema mbali ya mkuu wa mkoa kutoa msaada huo wa bati na Madawati wadau wengine waliofika kuchangia kituo hicho ni banki ya CRDB ambao wamesaidia fotari kwa ajili ya kujengea kituo hicho.

Kwa upande wake mkuu wa kituo hicho Padri Franco Soloberi alisema kuwa wamepata faraja kubwa sana kutokana na jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya mkoa wa Iringa kwa kituo hicho ,kwani alisema mkuu huyo wa mkoa alikuwa ni mtu wa kwanza kufika kusaidia kuzima moto na kusaidia msaada wa magodoro siku tukio hilo lilipotokea .


Aidha alisema msaada unaohitajika ni mkubwa kwani kituo hicho kinazaidia ya watoto 50 ambao kwa sasa hawana sehemu ya kulala baada ya jengo hilo kuungua moto.

Comments