Saturday, August 13, 2016

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAANDAA SEMINA KWA WAHARIRI WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR LEOMkuu wa Mawasiliano na Masoko mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa James Mlowe akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali na wageni waalikwa kwenye mkutano ulioandaliwa na LAPF,uliofanyika mapema leo jijini Dar Es Salaam.Mkutano huo uliokuwa na wawasilishaji mada mbalimbali walioelezea Mafanikio ya mfuko huo,Dira ya mfuko huo,mambo ya uwekezaji,nini ufanye ukipata pensheni yako mara baada kustaafu,mafao yanayotolewa na mfuko huo sambamba na pensheni mbalimbali ikiwemo pensheni ya Urithi,pensheni ya ulemavu na nyinginezo .

Meneja wa Kanda ya Dar Es Salaam kutoka mfuko wa Pensheni wa LAPF.Bi.Amina Kassim akiwasilisha mada iliyohusu Maandalizi ya kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu namna ya kutumia pensheni yako mara tu baada ya kustaafu katika mkutano kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania,mkutano huo wa siku moja uliondaliwa na LAPF umefanyika leo jijini Dar .Bi Amina alieleza kuwa kuna tafiti zinabainisha kuwa baadhi yao wakishapata fedha za kustaafu mara nyingi wamekuwa wakikosa nidhamu ya kuzitumia fedha hizo,wamekuwa wakinunua vitu vya anasa wasivyokuwa na ulazima navyo ,wamekuwa wakikosa ndoto kuhusu Maisha watakayoishi baada ya kustaafu,hivyo amewataka Wastaafu kuwa na mambo muhimu ya kufanya ikiwemo maandalizi ya kiuchumi,kuwa na nidhamu ya fedha,kuwekeza fedha zao katika mambo mbalimbali,kufanya uwekezaji wa biashara binafsi. 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri,Bwa.Theophil Makunga akitoa mwongozo mfupi kwa wageni waalikwa wa mkutano kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania,mkutano huo wa siku moja uliondaliwa na LAPF umefanyika leo jijini Dar,ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo nashughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.
Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor Kikoti akiwasilisha mada kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania, iliyokuwa ikihusu mambo mbalimbali ya mfuko huo ulioanzishwa mwaka 1944,ikiwa na Dira ya kuwa mfuko bora wa Pensheni unaopendwa zaidi hapa nchini.

Afisa Mwandamizi Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bi. Rehema Mkamba akitoa maelekezo mafupi kwa washiriki wa mkutano wa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania katika mkutano huo uliondaliwa na LAPF,uliofanyika jijini Dar.Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano huo uliondaliwa na LAPF .
Post a Comment