Wednesday, August 17, 2016

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) NA WENZAKE NANE WAFIKISHWA MAHAKAMANI


 
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine  nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea.

Mnamo mwezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo. .

No comments:

RAIS SAMIA AZINDUA HUDUMA YA SARATANI KCMC, AAHIDI USHIRIKIANO KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Tiba Mionzi (Radiothera...