Monday, August 22, 2016

HUYU HAPA NDIYE MKUU MPYA WA WILAYA YA ARUSHA ALIYETEULIWA NA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI


Mkuu wa Wilaya ya Arusha mteule Bw. Gabriel Fabian Dagarro




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 21 Agosti, 2016 amemteua Bw. Gabriel Fabian Daqarro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Bw. Gabriel Fabian Daqarro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mrisho Mashaka Gambo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Uteuzi wa Bw. Gabriel Fabian Daqarro unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
21 Agosti, 2016

No comments:

MMUYA: WANANCHI WANUFAIKE NA UWEKEZAJI WA NHC KUPITIA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maghala unaotekelezwa na S...