Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitembelea Kituo kikuu Ubungo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na sehemu ya Wananchi waliokuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Ubungo, Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasalimia wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wa jiji kuanza mchakato wa kuhamisha kituo kikuu cha mabasi ya mkoani cha ubungo kuhamia Mbezi mwisho
Makonda ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo hicho leo, amesema kituo hicho kimeelemewa na idadi ya kubwa ya wasafiri huku miundombinu haiendani na utoaji wa huduma kwa wasafiri wanaotumia kituo hicho.
Makonda amesema kuwa baada ya kituo hicho kuhama panatakiwa kufanyika uwekezaji wa soko kubwa ili kupunguza msongamano wa watu katika soko la Kariakoo.
Aidha Makonda amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuonekana kwa kituo hicho kuwa kidogo na kushindwa kutoa huduma ya usafirishaji ya abiria wanaoingia na kutoka katika mikoa mbalimbali.
Makonda ameutaka uongozi wa kituo hicho kufunga taa maeneo yote kutokana na kutawala kwa giza nyakati za usiku,ambapo ni hatari kwa usalama wa abiria wanaoshuka nyakati hizo.
RC Makonda pia amepiga marufuku kukamata magari kwa kigezo cha maegesho, wakati hakuna alama zinazoonyesha sehemu ya kuegesha magari.
Comments