Monday, February 01, 2016

RAIS MSTAAFU JK AKUTANA NA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA DKT. NKOSAZANA DLAMINI ZUMA


Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
Mheshimiwa Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.  Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na  kuwa tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.

SERIKALI KUJENGA VYUO VYA VETA KILA WILAYA

VETANaibu Waziri Elimu Wazira wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.
……………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.
Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGMZO NA RAIS UHURU KENYATA WA KENYA AU ADDIS ABABA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia, Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili masuala ya Usalama Barani Afrika ambapo Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
(Picha na OMR)

SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

KIGWAGALANaibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
…………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohammed Bakar(CCM) lililouliza kuwa bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa maswali na majibu,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kuhakikisha kuwa haki hizi zinapatikana,Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.
Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.
“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto” Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.
Serikali kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

1
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
3
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).
4
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
5
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani).
6
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

KUNDI LA MZIKI LA NAVY KENZO LATOA WIMBO NA VIDEO MPYA-KAMATI

THE INDUSTRY MUSIC LABEL
Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaitwa “Kamatia” , Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka, Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya ‘Flash Mob’ Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.
Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava, Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.
Kamatia ni wimbo ambao unaongelea kuhusu wapenzi wawili waliomua kushikana hasa kwenye mapenzi , Midundo ya nyimbo hiyo ina mahadhi ya Dancehall na vionjo vya kipekee kutoka kwa Producer bora Tanzania Nahreel.
Nahreel Ambaye ni mmoja wa Kundi la Navy Kenzo ni Producer wa Muziki bora Mwenye tuzo ya Kilimanjaro Music, Ametengeneza nyimbo mbali mbali zilitamba Kama Nana ya Diamond Ft Flavor,  Joh Makini Ft Aka Don’t Bother and Vanessa Mdee’s Nobody but me, Never ever na Hawajui, pia ndio mpishi wa Nyimbo ya Navykenzo ‘Game’
 Bonyeza Link ifuatayo Kudownload Wimbo huo ;DOWNLOAD AUDIO
au Angalia Video Hapa;VIDEOImetolewa na
The Industry
Email;bookings@navykenzo.com

MFUKO WA DHARURA WA UN WATOA DOLA MILIONI 11 KUSAIDIA WAKIMBIZI WA BURUNDI NA JAMII YA TANZANIA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania—ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miaka mingi—imetengewa dola za Marekani milioni 11 (Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24) kutoka katika kiasi hicho kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi.
liu
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa msaada katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara mkoani humo
Zaidi ya raia 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Tanzania hivi sasa ina zaidi ya wakimbizi 193,000. Kutokana na ukweli kwamba takribani wakimbizi 1,500 wanawasili nchini kila wiki, inabashiriwa kwamba huenda idadi jumla ya wakimbizi ikafikia 230,000 hadi mwisho wa mwaka 2016. Hali hii inasababisha changamoto nyingi hasa katika kutoa msaada na kinga ya kutosha kwa wakimbizi.
Mchango huu mkubwa kutoka CERF utakuwa muhimu sana katika kutoa misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, na vilevile kwa jamii za wenyeji ambazo zinahitaji kwa haraka huduma bora za maji safi, usafi wa kutosha, matunzo ya afya, chakula na makazi. Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kushughulikia mlipuko uliopo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeathiri mikoa 19 nchini. Fedha za CERF kwa hiyo zitasaidia kuhakikisha kwamba maeneo muhimu zaidi katika dharura yanafanyiwa kazi na kwamba wakimbizi wanapewa kinga na huduma za msingi.
Picture2
Baadhi ya wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma
“Shirika la Kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) linakaribisha mchango huu wenye ukarimu mkubwa kutoka CERF ambao unakuja katika kipindi mwafaka kabisa. Utoaji msaada kwa wakimbizi ulikuwa ukikabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka 2015, hali iliyoathiri sana uwezo wetu wa juhudi za pamoja katika mwaka 2015. Tuna imani kwamba hii ni ishara ya kwanza kwa upatikanaji wa fedha nyingi zaidi kwa utoaji msaada katika mwaka 2016. Kwa hakika, mchango huu utasaidia kuziba upungufu mkubwa uliojitokeza katika wito wetu wa sasa na hivyo kushughulikia mahitaji makubwa zaidi ya wakimbizi na jamii za wenyeji,” alisema Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Bi. Joyce Mends-Cole.
Kadiri mahitaji ya kiutu yanavyoongezeka, mchango kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa matumaini ya kuendelea kushughulikia dharura ya wakimbizi kutoka Burundi. Tangu mwaka 2006, Nchi 125 Wanachama wa Umoja wa Mataifa na waangalizi, wahisani kutoka sekta binafsi na serikali katika kanda zinazohusika wameendelea kuusaidia Mfuko huo hadi sasa. CERF hadi sasa imetoa jumla ya dola za Marekani bilioni 4.2 (US$ 4.2bn, sawa na shilingi za Tanzania trilioni 9) kwa miradi ya kiutu katika nchi 94. CERF hupokea michango ya hiyari katika mzunguko wa mwaka ili kutoa msaada wa kifedha kwa hatua za kiutu za kuokoa uhai. CERF inapata fedha zake kutoka kwa washirika wengi huku michango mingi zaidi ikitoka: Uingereza, Swideni, Norwei, Uholanzi na Kanada.

PSPF “YAVUNA” MAMIA YA WANACHUO WA UDSM NA TUMAINI KAMPASI YA DAR ES SALAAM, WAJIUNGA NA MPANGO WA PSS

Mwanamuziki nyota nchini Vanes Mdee, akiweka dole gumba
tayari kuchapa kwenye fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS),
wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF wakati wa kongamano lililowakusanya wanafunzi wa
kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara na kufanyika chuoni
hapo mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na mpango huo baada ya
kupata elimu ya faida za kujiunga na mpango huo. Wanaoshuhudia, kutoka kulia ni
Balozi wa PSPF, Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anayefanya
kazi zake Ulaya na Marekani, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS wa
Mfuko huo, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Rahma Ngassa.

No comments: