Wednesday, February 03, 2016

MKUTANO WA KUHIFADHI URITHI WA UTAMADUNI NA UBUNIFU VIWANDA KATIKA SEKTA YA UTAMADUNI WAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

H1
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi(aliyesimama) akifunga mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni uliokuwa na dhumuni la kuwajengea uwezo wasanii wa sanaa mbalimbali ili waweze kuhamasisha jamii katika kuwaletea maendeleo chanya.
H2
Washiriki wa mkutano wa urithi wa Utamaduni na ubunifu Viwanda katika sekta ya utamaduni wakimskiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi(hayupo Pichani) wakati alipokuwa akifunga mkutano huo jana jijini Dar es Salaam.
H3
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akipokea moja ya zawadi ya mfuko kutoka umoja wa nchi za ulaya (EU) kutoka kwa Afisa Miradi sehemu ya Uchumi na utawala kutoka umoja huo Bi Alexa DU PLESSIS wakati wa mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni jana jijini Dar es Salaam.
H4
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah kihimbi akiongea jambo na mkuu wa Idara ya uchumi na utawala kutoka umoja wa nchi za ulaya(EU).Bw.Olivier Coupleux wakati wa mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni uliokuwa na dhumuni la kuwajengea uwezo wasanii wa sanaa mbalimbali ili waweze kuhamasisha jamii katika kuwaletea maendeleo chanya.
H5
Post a Comment