Thursday, May 06, 2010

Rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua afariki



Rais wa Nigeria Umaru Musa Yar'Adua amefariki Dunia. Bw. Yar'Adua alifariki dunia saa tatu na nusu usiku wa Jumatano. Kiongozi huyo wa Nigeria alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Kifo chake kilitangazwa na kituo cha televisheni cha Nigeria, N.T.A

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho, kifo cha Bw Yar'Adua kilitangwa na msemaji wa Ikulu, Ima Niboro. Kaimu wa rais Goodluck Jonathan aliarifiwa punde baada ya kifo hicho kutokea na kuelezea kuhuzunishwa sana na taarifa hizo.

Yar'Adua atazikwa Alhamis alasiri nyumbani kwake katika jimbo la Katsina.

Kiongozi huyo wa Nigeria alipatwa na maradhi ya ini mwaka 2000, lakini akapuuza taarifa kuwa hali yake ya afya ilikuwa mbaya. Yar'Adua alipelekwa nchini Saudi Arabia kwa matibabu mwezi Novemba mwaka jana. Tangu wakati huo hajaonekana hadharani.

Naibu wake, Goodluck Jonathan, alichukua hatamu za uongozi kama kaimu mnamo mwezi Februari, tayari ameapishwa rasmi kama Rais mpya wa Nigeria. KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA

No comments:

CGP. KATUNGU AWATAKA MAAFISA USTAWI KUELIMISHA WAFUNGWA HAKI NA WAJIBU WAO

  Na. Ssgt Mawazo Mtondo – Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Ma...