Wednesday, May 05, 2010

JK: Bora tukose mapato Tuteketeze malaria



Tanzanian President Jakaya Kikwete (L) listens as Klaus Schwab, founder and chairman of the World Economic Forum , addresses delegates at the opening of the 20th World Economic Forum on Africa in Dar es Salaam May 5, 2010. REUTERS/Thomas Mukoya (TANZANIA - Tags: BUSINESS POLITICS)


************************************************************

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa ni bora Tanzania kukosa mapato, kuliko kupoteza maisha ya maelfu ya Watanzania wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa Uchumi Duniani (WEF), unawakutanisha washiriki kutoka nchi 85 duniani pamoja na mambo mingne unajadili namna ya kunyanyua uchumi wa Bara la Afrika hasa baada ya kukumbwa na msukosuko mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo, mkutano huo unakusudia kutoa changamoto na mapendekezo ya njia sahihi ya kupambana na kutokomeza kabisa ugonjwa huo namba moja kwa kusababisha vifo vya kina mama waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano duniani.

Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa hapo baina ya washiriki wa mkutano huo, Rais Kikwete alieleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza malaria nchini.

Moja ya mikakati hiyo ni kwa serikali kuzifutia ushuru bidhaa zote zinazohusiana na matibabu pamoja na mapambano dhidi ya malaria kuingia nchini, jambo ambalo baadhi ya Watanzania wanadhani huenda likaathiri pato la taifa.

Lakini Rais Kikwete akionekana mwenye furaha baada ya Tanzania kumwagiwa sifa katika mkutano huo kutokana na juhudi zake za kupambana na malaria.

“Lakini kama kuna maelefu ya Watanzania wanapoteza maisha kwa sababu ya malaria na tunaweza kuyaokoa basi ni afadhali tukose mapato, lakini tuokoe maisha ya Watanzania,”alisema Kikwete

Alisema licha ya mapambano dhidi ya malaria kuanza kwa muda mrefu nchini, lakini serikali yake inaona ndio kwanza yanaanza kutokana na umuhimu na haja kubwa iliyopo ya kutokomeza ugonjwa huo na hatimaye kuokoa maisha ya nguvu kazi ya Watanzania. Imeandikwa na Salim Said.

No comments: