Baadhi ya wadau mbalimbali Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali zililokuwa zikitolewa na viongozi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya utendaji kazi wa TAWLA hapa nchini.sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Aron Msigwa-Maelezo na Amour Nassor -VPO)
Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akizinduwa Mpango Kazi kwa mwaka 2010/ 2015 wa Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA), kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Umoja huo yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja huo Bibi Victoria Mandele, kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki ya Mwanamke ni haki ya Wote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanasheria Wanawake wa Tanzania (TAWLA) Bibi Victoria Mandale kutokana na kutambuwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza Umoja huo, katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA)zilizoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam, kauli mbiu ya mwaka huu ni haki ya Mwanamke ni Haki ya Wote.
Comments