Thursday, May 13, 2010

Ajali ya ndege yaua 104 Libya


Mabaki ya ndege aina ya Air Bus 330, iliyopata ajali

Maafisa nchini Libya wameripoti kuwa, ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli na kuua takriban watu 104.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa safarini kutoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Maafisa wamesema ilianguka wakati ikjaribu kutua karibu na uwanja huo.Takriban abiria 93 walikuwa ndani ya ndege hiyo pamoja na wafanyakazi kadhaa wa ndege hiyo aina ya Air Bus 330.

Watu hao wanaaminika kutoka mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Uingereza na Afrika Kusini.Wafanyikazi 11 wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa raia wa Libya.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London baada ya kusimama kwa muda mjini Tripoli.

Magari ya kuwabebea wagonjwa yameonekana kuelekea kwenye uwanja huo. Shirika la ndege la Afriqiyah lilianzishwa nchini Lybia mwaka wa 2001.

CHANZO: bbcswahili.com

No comments: