Sunday, March 29, 2009

Ajali mbaya ya treni yaua watu sita





HABARI zilizotufikia katika deski letu la Mzee wa Mshitu zinasema kuwa watu sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na treni ya mizigo Mpwapwa mkoani Dodoma jana.

Ajali hiyo ilisababisha mabehewa kadhaa ya terni hizo kuanguka huku baadhi ikiwemo lililobeba abiria kuharibika vibaya na kulazimu wataalam kutafutwa ili kulikata na kuokoa watu walio wazima au maiti ndani ya behewa hilo.

Mwananchi imefika eneo la ajali na kujionea hali halisi ikiwemo kushuhudia shughuli ya ukataji behewa hilo lenye abiria ndani ikifanyika kwa kusuasua kutokana na uduni wa vifaa vinavyotumiwa na mafundi wa Kampuni ya Reli (TRL) wakishirikiana na jeshi la polisi.

Hata hivyo hadi majira ya saa 10:15 jana maiti tano za abiria wote wakiwa wanaume zilikuwa zimeokolewa katika ajali hiyo, ambapo majeruhi walipekewa katika hospitali ya Mpwapwa kwa matibabu. Picha za mdau Faraja Jube.

No comments: