Michael Uledi afariki dunia



MWANDISHI Mwandamizi wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) aliyekuwa pia Mwakilishi wa kampuni hiyo Dodoma Michael Uledi,40, amefariki dunia jana.

Marehemu Uledi aliyefariki kutokana na maradhi ya kifua kikuu alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mirembe alikuwa akisumbulia na maradhi hayo kwa tangu miezi sita iliyopita. Ameacha mke na mtoto mmoja.

Uledi amefanya kazi katika kampuni ya MCL katika ofisi za Dodoma tangu mwaka 2007.

Alizaliwa mwaka 1969 katika kijiji cha Buigiri, Chamwino mkoani Dodoma, akapata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Buigiri kuanzia mwaka 1977 hadi 1983.

Baadaye alijiunga na shule ya sekondari Chidya wilayani Masasi mkoani Mtwara, kati ya mwaka 1986 na 1989.

Mwaka 1990 marehemu Uledi alifaulu na kujiunga na shule ya sekondari Moshi kwa masomo ya juu ya sekondari na alihitimu mwaka 1992. Baadaye alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ikosi cha Buhemba, mkoani Mara mwaka huo huo.

Comments