Machimbo ya kunduchi kibano mtindo mmoja




Mambo si mambo katika machimbo ya Kunduchi ambapo kichapo kimekuwa kikitembea mara kwa mara wachimbaji wametimuka na wengine kudinda kutoka lakini hivi sasa ulinzi mkali umeimarishwa katika machimbo hayo ili kuwazuia wachimbaji wasio na leseni wasiweze kuendelea kuchimba mahali hapo kwa kuwa wanaharibu mazingira.

Kuimarishwa huko kunatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la hivi karibuni la kuzitaka mamlaka husika kuwazuia wachimbaji hao na kuwachukulia hatua kali wale watakaokaidi agizo la kuondoka mahali hapo.

Katika taarifa yake, Rais Kikwete alizitaka Manispaa ya jiji kwa kushirikiana na Kinondoni kuwaondoa wachimbaji hao na kumtaka Kamishna wa madini kusimamia zoezi zima la kuwaondoa wachimbaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Karunguyeye alisema kuwa zoezi hilo litakuwa la kudumu mpaka wananchi hao watakapoacha kuchimba kokoto katika eneo hilo.

Comments