HARARE, Zimbabwe
WAZIRI Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai jana alijeruhiwa na mkewe kufariki kwenye ajali ya gari, kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya chama chake.
Msemaji wa chama hicho cha MDC, Nelson Chamisa alisema Tsvangirai alikimbizwa hospitalini, lakini akabainisha kuwa hakuwa kwenye hali mbaya. Alisema alikuwa akisubiri taarifa zaidi.
Habari nyingine kutoka ndani ya chama hicho zinasema kuwa mke wa Tsvangirai alifariki.
Tsvangirai ameunda serikali ya pamoja na Rais Robert Mugabe ambaye alitoa nafasi hiyo ili kuinusuru nchi kutoka katika matatizo ya kiuchumi.
Serikali mpya inakabiliwa na mlolongo wa matatizo: chakula na mafuta, mfumumo wa bei ambao umekuwa mkubwa kuliko wa nchi yoyote duniani na kuibuka kwa ubonjwa wa kipindupindu ambao umeambukiza zaidi ya watu 88,000, huku karibu watu 4,000 wakiwa wamepoteza maisha, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Wazimbabwe na nchi wahisani za Magharibi wanategemea serikali mpya itaimarisha uchumi baada ya vyama vikuu vya kisiasa vinavyopingana kukubali kugawana madaraka baada ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi Septemba.
Hali imekuwa tete kwenye serikali mpya baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa MDC, Roy Bennett.
Comments
Hata Waziri Mkuu wa Tanzania aliwahi kufa kwa ajali ya gari. Si unakumbuka ajali ya Dumisani Dube na msafara wa Hayati Edward Moringe Sokoine?
Achilia mbali hiyo ya hayati Sokoine. Msafara wa Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere uliwahi kugongwa na gari ya Muhindi maeneo ya Peugeot Motors
Tukirudi nyuma zaidi king'ora cha kuongoza msafara wa Waziri Mkuu Rashid Mfaume Kawawa kiliwahi kumgonga mtoto mitaa ya Ikulu.
Namshukuru Mungu jana Morgan Tsivangirai mwenyewe kajitokeza na kusema ilikuwa ni ajali. Nadhani vinginevyo ingekuwa kasheshe.