Tuesday, March 17, 2009

Rais wa Ravalomanana ajiuzulu






ANTANANARIVO, Madagascar

RAIS wa Madagascar Mark Ravalomanana amejiuzulu na kukabidhi nchi kwa jeshi la nchi hiyo baada ya sekeseke lililodumu ndani ya taifa hilo kwa muda sasa na baada ya kiongozi wa upinzani wa taifa hilo, Andry Rajoelina kuanzisha vuguvugu na kuungwa mkono na jeshi la taifa hilo na sasa ameingia katika ofisi maalum za rais wa nchi hiyo, siku moja baada ya kikosi cha skari wanaomuunga mkono kuziteka na kuzishikilia ofisi hizo.

Muda mfupi baada ya kuingia katika ofisi hizo, Rajoelina aliwaeleza wafuasi wake kuwa tayari mawaziri nane wa rais halali wa nchi hiyo, Mark Ravalomanana wamewasi.lisha kwake barua zao za kujiuzulu, baada ya kuona kwua mamlaka ya Ravalomanana imepoteza nguvu.

Rajoelina ameiongia katika ofisi hizo za rais katika majengo hatyo yaliyoshikilwia na askari wanaomtii, huki umbali wa kilomita 12 kutoka mji mkuu Antananarivo, Rais Ravalomanana amejifungia katika kasri jingine la rais huko Iavoloha, akizungukwa na kikosi chake maalum na baadhi ya wafuasi wake.

Ravalomanana tayari amepuuza woto na ushauri kutoka wka watu wake wa karibu kumtaka akimbilie uhamishoni na kupinga kung'atuka, huki akieleza kuwa atatetea haki yake hadi kufa, huku walinzi na wafuasi wake wakiwa wamezifunga njia zote zinazoelekea eneo hilo.

"Rais ameamua kusalia Madagascar, ameshawaambia walinzi wake waliomshauri akimbilie uhamishoni kuwa tatetea haki hata ikibidi mpaka kufa. Hii inaelekea kuwa njama ya mapinduzi ya kijeshi,” msemaji wa ofisi ya rais Ravalomanaan alieleza.

No comments: