Tume ya Rais ya kuchunguza ufisadi yaanza kazi

Na Tausi Mbowe

TIMU iliyoteuliwa kufuatilia taarifa ya ukaguzi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu upotevu wa fedha za akaunti ya Malipo ya Kigeni (EPA) imeanza kazi yake rasmi na tayari timu hiyo imeshaanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Time hiyo iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufutia kampuni ya Ernest & Young kubaini kuwa kulikuwa na upotevu wa zaidi ya Sh133 bilioni katika mazingira ya kutatanisha ndani ya benki hiyo na hatimaye Rais Kikwete kutengua wadhifa wa aliyekuwa Gavana Mkuu, Daud Balali.
Timu hiyo yenye wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za polisi ilipewa muda wa miezi sita kumaliza ukaguzi huo.
Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni Mwenyekiti wa Timu hiyo, Johnson Mwanyika ilisema tayari timu hiyo imeshaanza kazi yake na wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa wa wananchi.
Mwanyika alisema wananchi wote ambao mpaka sasa wamejitokeza wamejitokeza kwa ridhaa yao na kutoa taarifa muhimu zianzoendelea kusaidia kazi yao.
Timu hiyo imesema kuwa itakuwa makini kwa nia ya kuhakisha kuwa ukweli unajulikana na kuweka wazi hadharani ili kulinda heshima ya Taifa kwa kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini.
Kwa mujibu wa Mwanyika nia ya timu ni kufanya kazi yake kwa uhakika na kuwaomba wananchi kuwa na subira na kutoa kila ushirikiao utakaoiwezesha timu hiyo kukamilisha majukumu yake.
Alisema timu hiyo itaweza kufanikisha majukumu yake kama wananchi wote popote walipo wataendelea kuisaidia kwa kutoa taarifa zozote mbazo wataona ni muhimu na zinahusiana na kazi hii.
Alisema kwa sasa Timu hiyo imeweka utaratibu wa kupokea tarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya upambana na kuzuia rushwa na kutoa namba za simu za mikononi kwa wajumbe wa timu hiyo.
Wajumbe wengine katika timu hiyo ni pamoja na Mkuuwa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Saidi Mwema, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Lilian Mashaka. Wakati timu hiyo ikitangaza kuanza kazi yake rasmi tayari serikali kupitia Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji imesema ufisadi wa mabilioni ya shilingi uliobainika katika Akaunti hiyo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umepoteza imani ya wananchi kama chombo thabiti na makini katika utekelezaji wa majukumu yake.
Tayari serikali imeshatangaza bodi mpya ya benki hiyo ambayo inaongozwa na Gavana mpya wa BoT, Profesa Benno Ndulu, Mbali na Profesa Ndulu ambaye ni mwenyekiti, wajumbe wengine wa bodi hiyo ni pamoja na Manaibu Gavana, Dk Enos Bukuku, Juma Reli na Lila Mkila.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Meghji aliitaka bodi kuhakikisha inachukua hatua madhubuti kurejesha imani miongoni mwa wananchi kutokana na taarifa za kuhusika kwa BoT katika malipo haramu au ambayo uhalali wake unatia shaka, ikiwa ni moja ya mikakati ya bodi hiyo ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili.
Pamoja na mambo mengine bodi hiyo imepewa jukumu la kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya maofisa watakaodhihirika kuhusika na upotevu wa fedha za umma chini ya EPA kama ilivyoelekezwa na Rais Jakaya Kikwete na kuweka taratibu madhubuti ili kuepuka upotevu kama huo kutokea tena katika siku zijazo.
Vilevile, bodi hiyo imepewa jukumu la kuimarisha mfumo wa usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha, kuhakikisha usalama na umadhubuti katika mfumo mzima wa sekta ya fedha, kuimarisha masoko ya fedha na mkakati wa kuweka mazingira bora ya kisheria ili kuwezesha upatikanaji zaidi wa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa ajili ya sekta ya uzalishaji.

Comments

Anonymous said…
Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
Ingia website hizi uone.
http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
http://sunray22b.net/slavery.htm,
www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.