Wednesday, January 16, 2008

Mhariri Kubenea arejea nchini





Picha zote na Felix Fidelis

KAMANDA Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, aliyekuwa amelazwa hospitali nchini India akipatiwa matibabu ya macho, amerejea nchini na kudai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, wakiwamo vigogo wa serikali kwamba, ndio waliohusika na kushambuliwa kwake.

Kubenea (37)amesema anaamini hivyo kwa kuwa tukio la kushambuliwa kwake lilitokea katika mazingira ya kazi yake na pia baada ya moja ya magazeti yake kuyaweka majina na picha za watuhumiwa hao hadharani.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.

"Suala, hapa kuna mkono wa mtu. Wanaweza kuwa viongozi wa serikali kwa kuwa wapo baadhi yao walituhumiwa kuhusika na ufisadi na gazeti langu likaweka hadharani majina yao na pia wanaweza kuwa watu wengine," alisema Kubenea.

No comments:

KAMISHNA BADRU ATAKA UBUNIFU ILI KUENDELEZA MAPANGO YA AMBONI

KAMISHNA BADRU ATAKA UBUNIFU ILI KUENDELEZA MAPANGO YA AMBONI  Na Hamis Dambaya, Amboni Tanga. Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ng...