Friday, January 11, 2008

Kenya hakukaliki tena

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement (ODM), kimepanga kufanya maandamano makubwa ya siku tatu mfululizo kupinga matokeo yaliyomtangaza Rais Mwai Kibaki kuongoza tena katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

Tangazo hilo linafuatia juhudi za kimataifa za kutaka suluhu baina ya pande mbili zinazovutana zilizofanywa na Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika (AU), ambaye ni Rais wa Ghana, John Kufuor kushindikana.

Raisi Kufuor aliondoka mjini Nairobi juzi huku akishindwa kukutana na kufanya mazungumzo hayo ya kuleta amani baina ya Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki.

Mpaka sasa zaidi ya watu wanaokadiriwa kufikia 600 wameripotiwa kupoteza maisha katika ghasia hizo zilizotokea katika sehemu mbalimbali ya nchi hiyo.

No comments:

RUZUKU YA SH.MILIONI 250 YATOLEWA KWA WABUNIFU WA MATUMIZI BORA YA NISHATI

📌 Kamishna wa Umeme asema Serikali itaendelea kuwawezesha vijana wabunifu katika teknolojia ya matumizi bora ya nishati 📌 Wabunifu wa kike...