Tuesday, January 01, 2008

Wazungu wamkalia kooni Kibaki

ULE ujanja wa kishetani uliofanywa na Mwai Kibaki, Rais wa Kenya aliyejinyakulia uongozi wa kutangazwa na hatimaye kuapishwa umeanza kumtokea puani baada ya mataifa ya Magharibi kupinga matokeo ya kura za uchaguzi wa Kenya yaliyompa ushindi kuongoza nchi hiyo katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Waangalizi wa Kimataifa kutoka Jumuhia ya Ulaya wametoa tamko lao na kuelezea uchaguzi huo ulikuwa na kasoro kubwa.
Waangalizi hao walisema kuwa Rais wa Kenya hakupatikana kihalali na kwamba matokeo hayo hayakukidhi viwango vya kimataifa. Soma habari hii katika shirika la AFP kwa taarifa zaidi.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...