

Spika Marende


Hapa jamaa walikuja juu wakakataa kabisa kuibiwa

Hapa jamaa walikuwa tumbo joto

CHAMA cha ODM kimafanikiwa kuliteka Bunge la Kenya, baada ya Mgombea wake wa kiti cha Uspika Kenneth Marende kuibuka mshindi wa nafasi ya Spika wa Bunge ka nchi hiyo.
Katika uchaguzi huo uliokuwa wa vuta nikuvute, huku Mrende akiongoza mizunguko miwili ya kwanza, hatimaye aliibuka mshindi baada ya kushinda kura 105 dhidi ya kura 101 za mpinzani wake, Francis Kaparo aliyekuwa akitetea nafasi yake.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwa zaidi ya saa nne, Kenneth Marende aliteuliwa chini ya Chama cha ODM na Francis Kaparo aliteuliwa na chama cha PNU.
Kufuatia ushindi huo, hiyo inaweza kuwa hatua ya kwanza kwa PNU kupata nguvu ya kudhihirisha madai yao ya awali, wakimtaka Rais Kibaki kuondoka madarakani kwa tuhuma kuwa aliiba matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Disemba 27.
1 comment:
Hongera Wakenya.Hili ni funzo kwa Watanzania.Tusipojenga bunge lenye uwiano mzuri kati ya chama tawala na vyama shindani,tutalalamikia bunge milele,tuanze sasa.
Post a Comment