Tuesday, January 29, 2008

Kenya hakukaliki tena

Askari wa kuzuia ghasia wakiwazuia Wakikuyu baada ya kuzuka mapambano baina ya Wajaluo na Wakikuyu mjini Naivasha.

Mmoja wa wakazi wa Naivasha kutoka kabila la Wajaluo akimtoa motto kutoka katika gari la polisi katika eneo la Naivasha Club, mjini Naivasha.

Wakazi wa mji wa Naivasha, Kenya kutoka kabila la Kikuyu wakichoma mali za wenzao wa kabila la Wajaluo baada ya kuzuka katika mji wa Naivasha uliopo kilomita 60 nje ya jiji la Nairobi jana. Mapambano kadhaa yaliripotiwa kuibuka Magharibi mwa Kenya na makundi ya watu wenye silaha za kijadi kama mapanga na marungu walifanya vurugu katika mkoa wa Rift Valley baada ya wenzao kadhaa kupoteza maisha katika maambano ya kikabila na hivyo kurudisha nyuma juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan. REUTERS.



Wakikuyu wakinyanyua silaha zao za kijadi juu nje ya klabu ya Naivasha mjini Naivasha.


No comments:

MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TEWW

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2025 ni mgeni rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu y...