kikwete awaomgoza waombolezaji katika mazishi ya meja generali Marwa

Na Beldina Nyakeke, Musoma

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwte jana aliwaongoza waombolezaji katika mazishi ya laiyekuwa meja generali wa jeshi Michael Marwa (78) katika kijiji cha mogabiri wilayani tarime mkoa wa Mara.

Akizungumza katika mazishi hayo msahuri wa rais katika masual ya kijeshi nchini Uganda Generali Elly Twimine alisema kuwa nchi yake inata,mbua na kuelewa ushirikano uliopewa na nchi ya Tanzania wakati wa vita vya Kagera ambapo marehemu Marwa alikuwa miongoni mwa askari waliokwenda katika mapambano.

Generali Twimine aliwataka watanzaia kuungana pamoja na nchi zingine za afrika Mashariki ili kuleta maendelo katika nchi hizo na kuwataka waendelee kudumisha amani na utulivu ulioko nchini.

Alisema kuwa watanzania wanapaswa kuiga mfano wa tabia ya marehemu meja generali Marwa ambaye alikuwa msatri wa mbele katika kutete nchini yake hali ambayo alisema kuwa ndiyo iliyosababisha awe msatri wa mbale katika vita vya Kagera ili kuhakikisha kuwa wanamuondoa mduli Idd Amin katika utawala wa kidikteta nchini Uganda.

Marehemu alizaliwa mwaka 1930 katika kijiji cha Mogabiri wilayni Tarime ambapo laiitumikia jeshi la wanachi kwa kipiondi cha Miaka 37.

Alifariki januari 7 mwaka huu nchini afrika Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Medi-clinic,ameacha wajane saba na watoto 54.

Rais Kikwete aliongozana na mkwew mama salma Kikwtew katika mazishi hayo ambapo viuongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Mkuu wa majeshi nchini Jenerali David Mwamunyange, Wazii wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa. Prof. juma Kapuya, Mjane wa baba wa taifa mama Maria Nyerere pamoja naibu waziri ww miundombinu Dk. Makongoro Mahanga

Akihubiri katika mazishi hayo Adkofu mkuu wa Kanisa la Evangelical, Moses Kulola aliwataka watanzania kuoga tabia ya marehemu kwa maelezo kuwa alikuwa ni mtu mpenda amani na aliyewapenda watu wote bila ubaguzi.

Aidha aliwataka watanzania kumuomba Mungu ili amani na utulivu viweze kuendelea nchini.

Comments