Zuma azidi kung'ara

Wamemfanyia kila aina ya fitna ili kusudi akwame na wala asiweze kuiongoza taifa tajiri la kusini mwa Afrika la Afrika Kusini, lakini sasa Chama tawala cha nchi hiyo cha ANC kimeamua kumteua Jacob Zuma kuwa kugombea Urais wa chama hata kama anakabiliwa na tuhuma.

Anakabiliwa na tuhuma za ufisadi katika uuzaji vifaa vya kijeshi, na mikasa mingine kadhaa.

Halmashauri Kuu (NEC) ya chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, imempendekeza Jacob Zuma (65) kuwa mgombea wake wa kiti cha urais baada ya Rais Thabo Mbeki.

Zuma amethibitishwa kugombea kiti hicho mwakani baada ya Rais Thabo Mbeki, kumaliza muda wake. Hata hivyo, kamati kuu ya chama hicho itapaswa kukaa na kujadili suala hilo.

NEC ya ANC, ilimthibitisha Zuma na kusema imefanya hivyo nikjua kwamba anakabiliwa na tuhuma rushwa na kesi yake iko mahakamani, lakini wako nyumba yake.

Katibu Mkuu ANC, Gwede Mantashe alisema chama hicho kina muunga mkono kiongozi huyo katika kukabiliana tuhuma za rushwa zinazomkabili.

Comments