Hapa washikaji unaweza kuwaona kutoka kulia Danny Lyimo, Luwaga Kizoka, James Kapaya, Daudi Masoli na Mzee Gombo mvua ilikuwa imenyesha kinoma.
Yahya Charahani, Danny Lyimo na Luwaga Kizoka
Kumbukizi ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita: Safari ya Kimasomo na Ukumbusho wa Walimu
Picha hii ni kumbukumbu adhimu ya jopo la wanafunzi wa kidato cha sita miaka hiyo, wakiwa pamoja na walimu waliowaongoza katika safari yao ya elimu.
Katika kundi hili, tunamuona Kamanda Albert Ballati, aliyesimama karibu na mwalimu aliyekuwa maarufu shuleni kwa jina la Mwalimu Nyanda, mwalimu wa Baiolojia aliyewahi kuwahamasisha wengi kufahamu na kupenda somo hilo.
Mbele kabisa katika picha hii, anaonekana Afande Warioba, mwanafunzi aliyekuwa na nidhamu kali na anayekumbukwa kwa msimamo wake thabiti. Ingawa wakati huo alionekana kuwa mkali kwa wenzake, ni wazi kwamba alichangia katika malezi ya kimaadili na nidhamu miongoni mwa wanafunzi wenzake. Hali hii inazua swali la wapi alipo sasa na ni njia gani aliyochukua baada ya kuhitimu elimu yake.
Picha kama hizi huamsha kumbukumbu za maisha ya shule, urafiki uliodumu, changamoto zilizokuwepo, na mafunzo yaliyopatikana darasani na nje ya darasa.
Ni ushahidi wa safari ya pamoja iliyowajenga wengi, ikiwemo mafunzo ya nidhamu, uvumilivu, na juhudi za kutafuta elimu kwa bidii. Bila shaka, kwa waliokuwepo enzi hizo, hii ni kumbukumbu ya nyakati ambazo hazitasahaulika. Hapa ni langoni mwa Tabora boys high school, ukiwa unaingia hapa lazima uingien kikakamavu.
7 comments:
Namuona afande Warioba na mwanya wake hapo mbele...Duh,yaani Cherahani umenikumbusha mbaaaali sana.Kumbe Mzee nawe ulipita hapo?Katika hizo picha namkumbuka Lyimo,yuko wapi huyu?
Bonge
Charahani wawakumbuka kina Gilbert Mwoga, Godfrey rweyemamu, Kin Kizito waliokuwa mwaka mmoja mebele yenu??
Yesss Evarist kumbe unamkumbuka huyu afande alikuwa mnoko kichizi siku moja katupiga extea drilll pale smart area tlikoma ni dakika 15 kila mtu alikuwa akitambaa kwa mikono. Yesss nilipita pale bwana shule yetu ile nimeikumbuka ile mbaya. Lyimo yuko hapa Bongo.
Wenu namkumbuka sana Mwoga na taarifa nilizo nazo ni kwamba yuko Marekani sijui state gani. Kizito naye pia naambiwa yuko Marekani muda mrefu tangu amalize skuli tuuu. , Geofrey rweyemamu nimewahi kukuona hapa Dar.
Yesss Evarist kumbe unamkumbuka huyu afande alikuwa mnoko kichizi siku moja katupiga extea drilll pale smart area tlikoma ni dakika 15 kila mtu alikuwa akitambaa kwa mikono. Yesss nilipita pale bwana shule yetu ile nimeikumbuka ile mbaya. Lyimo yuko hapa Bongo.
Wenu namkumbuka sana Mwoga na taarifa nilizo nazo ni kwamba yuko Marekani sijui state gani. Kizito naye pia naambiwa yuko Marekani muda mrefu tangu amalize skuli tuuu. , Geofrey rweyemamu nimewahi kumuona hapa Dar.
Namtafuta Daudi Masoli tumepotezana miaka kama miwili,kama kuna mtu anajua habari zake tafadhali tuwaliane nae...
Hata mimi namkumbuka makarateka Warioba,Afande huyu mtaalamu wa viungo alikuwa chachu katika kuchakachua utukutu sugu....... Ingawa alionekana mtulivu wakati akitoa somo la miondoko,ikiwamo ghost walk......Alikuwa akiwachenjia kinoma wateja wa gatundu
Ha ha ha, Nilipita hapo mwaka 1986-1989, KMN
Post a Comment