Barua ya wazi kwa Marais Kikwete, Kagame na Kaguta juu ya hali ya Wakenya
Ninashindwa kuwasalimia kwa kheri za mwaka mpya. Katika eneo letu hili la Afrika, hakuna heri, kuna shari tu. Waafrika wenzetu huko Kenya wanakufa bila sababu. Sababu ni moja tu – uchu wa madaraka. Inanishangaza sana kwamba nyie kama viongozi wa nchi za Afrika zinazoshirikiana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye lengo la kujenga msingi wa Shirikisho la Afrika, mko kimya. Huu sio wakati wa kucheza mchezo wa kidiplomasia.
Hatutaki, hatutaki kabisa kuona tena jangwa la maauaji ya halaiki yatokee barani Afrika. Tumechoka kuona wanaadamu, Waafrika wenzetu, wakiuawa kama wanyama mitaani na hao wanaojiita eti vyombo vya usalama. Usalama wa nani kama sio wa wananchi?
Jukumu la awali kabisa la vyombo hivyo ni kulinda usalama wa raia; kutuliza ghasia sio kuchochea ghasia au chuki. Wakiwakuta waandamaji bila silaha wawalinde, wawashauri kufanya maandamano yao kwa amani, wawapatie nafasi ya kuonyesha madukuduku yao kuhusu uchaguzi. Bonyeza hapa upate kusoma uchambuzi huu zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...

-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
(Picha na Yahya Charahani) Kwa wale waliokulia maeneo haya, hili ni jambo la kawaida ukitoka mjini, shambani sijui hadi wapi kote ni haya h...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
No comments:
Post a Comment