Monday, August 03, 2026

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE 2026 DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili na kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane kwa mwaka 2026 yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Malecela Jijini Dodoma. Makamu wa Rais ni mgeni rasmi katika Siku Maalum ya Ushirika na Maadhimisho ya Miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inayofanyika leo tarehe 03 Agosti 2026 katika Maonesho ya Nane Nane Dodoma.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 3 Agosti 2026 amewasili katika Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma, yanakofanyika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane 2026.

Baada ya kuwasili, Mhe. Dkt. Nchimbi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea teknolojia, tafiti, bidhaa na huduma zinazotolewa na taasisi pamoja na wadau wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Makamu wa Rais ni mgeni rasmi katika Siku Maalum ya Ushirika na Maadhimisho ya Miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), yanayofanyika leo ndani ya Maonesho hayo.

Ushiriki wake unaendelea kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuimarisha ushirika, utafiti, matumizi ya teknolojia na ubunifu ili kuongeza tija na kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

#Nanenane2026 #Dodoma #Ushirika #TARI #KilimoChaKisasa

No comments:

NIRC YAFUNGUA SURA MPYA YA KILIMO: MIRADI 30, PAMPU 2,000 NA AJIRA 4,000

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inatarajia kuanza utekelezaji wa miradi mipya zaidi ya 30 ...