Monday, August 21, 2017

MADEREVA KITUO CHA SIMU 2000 WAGOMEA TOZO YA 1000

Mpiga picha wa Globu ya Jamii mapema leo asubuhi amekumbana na adha ya usafiri,kufuatia Madereva katika kituo cha mabasi simu 2000 Manispaa ya Ubungo jijini Dar kugoma kutoa huduma ya usafiri,kwa kile walichodai kupandishiwa tozo kutoka shilingi 500 hadi 1000.

Akizungumza zaidi mmoja wa Madereva wa dala dala katika mgomo huo (hakutaka kujitambulisha jina),alisema kuwa wao hawawezi kulipa tozo hiyo wakati miundombinu ya kituo hicho si rafiki na hairidhishi kabisa kwa vyombo vyao vya usafiri.

"ni vyema wakazirekebisha kwanza changamoto kadhaa zilizopo hapa kituoni,kisha baadae waje na huo mkakati wao wa kutupandishia hiyo tozo yao,lakini kwa sasa itakuwa vigumu kulipa kwa sababu kama unavyoona mazingira yalivyo hapa kituoni",alisema mmoja wa Madereva.

Mpiga picha wa Globu ya Jamii pamoja na kuonja joto ya jiwe ya kukosa usafiri,pia alijionea adha waliokuwa wakiipata abiria wengine waliokuwepo kituoni hapo,huku baadhi ya abiria wakilazimika kutumia usafiri wa piki piki kuwahi kwenye shughuli zao na wengine wakitembea kwa Miguu. 

Mpaka Globu ya Jamii inaondoka kituoni hapo ufumbuzi bado ulikuwa haujapatikana.
 Madereva na Makondakta wakijadiliana kufuatia mgomo huo
Baadhi ya mabasi (dala dala) yakiwa yamepaki kituoni hapo yakisubiri mgomo huo upatiwe ufumbuzi. 
 Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri kituoni hapo mapema leo asubuhi

No comments: