MCHENGA BBALL STARS YAFUFUA MATUAMINI YA UBINGWA SPRITE BBALL KINGS

Nahodha wa Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph akitaka kumtoka nahodha wa kutoka TMT, Isihaka Maoud katika mchezo wa fainali ya tatu ya Michuano ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa Mchenga kushinda kwa lama 87-82 dhidi ya TMTmchezo uliochezwa katika Viwanja vya Don Bosco OysterbayJijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchezo wa tatu wa Fainali ya michuano ya mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings imeendelea mwishoni mwa wiki kwa timu ya TMT kukubali kipigo cha pili kutoka kwa wapinzani wao Mchenga BBall Stars wakilipa kisasi kwa alama 87-82 dhidi ya TMTmchezo uliochezwa katika Viwanja vya Don Bosco OysterbayJijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa fainali ya kwanza, Mchenga walifanikiwa kutoka na ushindi wa alama 101-70 vya TMT, lakini fainali ya pili TMT waliweza kujibu mapigo na kuwaadhibu mahasimu wao kwa alama 82-78 dhidi ya Mchenga. 

Kwenye mchezo huo, Mchenga walianza kwa taratibu huku TMT walionekana wako vizuri sana katiia idara zote ikiwemo ulinzi na ushambuliaji lakini mpaka robo ya kwanza inamalizika Mchenga walikuwa wanaongoza ila katika robo ya nne na ya mwisho umakini wa TMT uliweza kuwafanya waanze kutawala mchezo huo na kuepelekea Mchenga kupata ushindi katika sekunde za mwisho wa mchezo huo. 

Kutokana na matokeo hayo timu ya Mchenga BBall Stars imeweza kurudisha furaha kwa mashabiki zao baada ya kupoteza mechi iliyopita katika fainali hizi za Sprite BBall Kings kwa kuchapwa kwa pointi 87-78 na mpinzani wake TMT.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweza kuonyesha utofauti mkubwa katika mechi zote zilizowahi kuchezwa katika michuano hii, kutokana na wachezaji wa pande zote mbili kuonyesha umahili wao waliyokuwa nao katika kucheza pamoja na kushambulia. 
Mamia ya mashabiki waliyoweza kujitokeza kutazama mtanange wa fainali za Sprite BBall Kings leo Don Bosco Oysterbay 

Kwa upande mwingine, mchezaji Erick Lugora kutoka TMT ameweza kuibuka 'best scorer' kwa pointi 23 akifuatiwa na Marcelo Nyirabu kutoka Mchenga BBall Stars kwa kupata pointi 18 katika mechi ya tatu ya fainali za Sprite BBall Kings. 

Mchenga na TMT zitakutana tena Agosti 23 (Jumatano) ya mwaka huu kucheza game 4 ambapo mchezo huo kwa upande mmoja utaweza kuwa wa mwisho endapo Mchenga BBall Stars akiweza kufunga tena na bingwa wa Michuano ya Sprite BBall Kings 2017 atajinyakulia kitita cha shilimgi Milioni 10 huku mshindi wa pili akipata Milioni 3 na mchezaji bora wa michuano hiyo (MVP) akizawadiwa milioni 2.

Michuano ya Sprite BBall Kings ilianza mapema Mwezi Mei na iliweza kusaili timu 56 na kuanza hatua za mtoano mwezi June katika Viwanja mbalimbali na imechukua takribani miezi mitatu kufikia Fainali, kwa mujibu wa waandaaji michuano hii itakuwa ni endelevu na wanatarajia mwakani kupata timu nyingi zaidi zitakazoshiriki. 
Patashika uwanjani.
Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu Nchini Marekani Hasheem Thabeet alikuwa moja ya watazamanji katika Viwanja vya Don Bosco OysterbaY.

Comments