MAONESHO YA NANE NANE 2017 MKOANI LINDI: MHANDISI METHEW MTIGUMWE ASEMA MAONESHO HAYA NI TASWIRA CHANYA KWA WAKULIMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. (Picha zote na Mathias Canal)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akizungumza jambo wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe alipotembelea kitalu cha Mikorosho wakati wa  Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Ukanda wa Tropiki (IITA) wakati wa Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Ukanda wa Tropiki (IITA) wakati wa Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe alipotembelea mashamba darasa ya mazao mbalimbali wakati wa  Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe alipotembelea mashamba darasa ya mazao mbalimbali wakati wa  Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe alipotembelea shamba darasa la mikorosho wakati wa  Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Na Mathias Canal, Lindi

SHEREHE za wakulima maarufu kama Nane Nane zimetajwa kuwa ni darasa huru kwa wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla kwani zinatoa nafasi kwao kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kilimo chenye tija, Ufugaji wa kisasa na Uvuvi wenye tija pasina kuharibu rasilimali za serikali.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Alisema kuwa serikali inatambua kadhia inayowakabili wakulima nchini ikiwemo pembejeo feki ambazo wakulima wanauziwa, hivyo kupata hasara ikiwamo mazao kidogo na hafifu tofauti na kusudio lao la kujipatia mazao mengi ya biashara na chakula jambo ambalo inalifanyia kazi ili kukabiliana nalo kwa haraka.

Maonyesho haya Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi yatawasaidia wakulima kupata elimu juu ya pembejeo halisi ikiwamo mbegu, dawa (viuatilifu), mbolea kutoka kwa mashirika husika yanayozalisha pembejeo mbali mbali, ili kuwasaidia kuepuka kununua pembejeo feki ambazo huwasababishia hasara na kuwakatisha tamaa.

Sherehe hizi huambatana na maonyesho ya bidhaa za kilimo yanayofanywa na wakulima na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo, lengo likiwa ni kujitangaza shughuli zao, kubadilishana uzoefu na wataalamu wa kilimo.

Pia wakulima wadogo ambao ni wengi ukilinganisha na wakulima wakubwa watajifunza mbinu mpya za kitaalamu za kilimo zinazoendana na wakati uliopo kwa maana ya mabadiliko ya kiteknolojia na tabia nchi ili wakulima waweze kulima kilimo cha kisasa na kunufaika kiuchumi.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea ambacho hakizingatii kanuni za kitaalamu, jambo lililowasababisha kukata tamaa na kuona kuwa kilimo hakilipi kutokana na mbinu duni walizozitumia.

Alisema kuwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi inajipambanua zaidi kumkwamua mkulima ili Wakulima nchini waondokane na kilimo cha kubahatisha cha kutegemea mvua na badala yake wajikite katika kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika, kinachoweza kuyabadilisha maisha yao kiuchumi kutokana na mazao mengi watakayopata.

"Natambua kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanategemea sekta ya kilimo kama ajira yao Sehemu kubwa ya kilimo ni cha wakulima wadogo wadogo ambao mashamba yao yana ukubwa wa hekta 0.9 na hekta 3.0 kwa kila moja, Karibu asilimia 70 ya ardhi ya kilimo na mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono, asilimia 20 hutumia maksai na asilimia 10 hutumia trekta Hivyo kama wizara tutajitahidi kadri iwezekanavyo kuwakwamua wananchi ili kuondokana na uduni katika mavuno" Alisema Mtigumwe

Mbali na hayo, kilimo cha Tanzania ni cha kutegemea mvua, uzalishaji wa mazao ya chakula ndio unaongoza katika uchumi wa kilimo. Hekta milioni 5.1 zinalimwa nchi nzima kila mwaka, kati ya hizo asilimia 85 ni kwa ajili ya mazao ya chakula tu, na wanawake ndio wafanyakazi wakubwa mashambani.
Mhandisi Mtigumwe anasema katika maonesho hayo anatarajia wakulima watajifunza mbinu bora na za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Aidha ametoa  wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.

Comments