Monday, August 14, 2017

Airtel yang’ara ripoti ya TCRA



· Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu 
· Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money wasajiliwa 

Airtel Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania ambayo imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku makampuni ya simu za mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji wa huduma za kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA). 

Kulingana na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly Communication Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania yaliongeza watumiaji wapya wa huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi cha April mpaka Juni. 

Kutokana na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya 1,038,193. Hii inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa huduma za kifedha za simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa suluhisho sahihi kwa huduma za kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa Tanzania. Kwa mfano tuangalie huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa kupitia Airtel Money, hatimaye imeanza kuzaa matunda’. 

Huduma ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa suluhisho inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia inaenda samba samba na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara wadogowadogo na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema Singano. 

Ikiwa na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina jumla ya wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya makampuni matano ya simu za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel Tanzania pia imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya mwaka na hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia 40.358 milioni mwishoni mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi mwaka huu. 

Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi nchini kwa mujibu wa Singano anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua vizuri huku kampuni hiyo ikiendelea kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja wengi wapya. 

Moja ya mradi mkubwa wa uwekezaji ni mradi wa U900. Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta kuboresha miundombinu ya kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na kuboresha kasi ya data 

"Hii mikakati yetu ya kuimarisha maisha ya Tanzania kupitia huduma za kidigitali. Katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari yamebadilishwa, mpango wetu ni kueneza mradi wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika masoko mengine yenye uwezo mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza Singano.

No comments: