Wednesday, August 30, 2017

Dawasa kujenga miundombinu ya majitaka jijini Dar es Salaam

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, Mhandisi Romanus Mwang’ingo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati Dawasa ya maji safi na majitaka jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maelezo, Rodney Thadeus kulia ni Meneja Mawasiliano Dawasa, Neli Msuya.
Meneja wa Mawasiliano wa Dawasa, Neli Msuya akizungumza juu miradi inajengwa na Dawasa katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam na Sehemu ya mkoa wa Pwani  jijini Dar es Salaam.

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

UZALISHAJI wa Maji Safi kunahitaji kuwepo na miundombinu ya maji taka ambayo yanazalishwa na maji safi katika kutunza mazingira pamoja na afya kwa wananchi wanatumia maji safi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, Mhandisi Romanus Mwang’ingo amesema kuwa wameanza kufanya utekelezaji wa miradi ya ukusaji na uondoshaji wa majitaka kwa kuanzisha miradi mitatu ya kisasa ya kusafisha majitaka hayo.

Amesema Miradi hiyo itakwenda sambasamba na uzalishaji wa mabomba ya kukusanya majitaka hayo kwa kujenga miundombinu katika maeneo ya Jangwani, Mbezi Beach pamoja na Kurasini.

Mwandisi Mwang’ingo amesema ujenzi wa miundombinu hiyo itaongeza kiwango cha kusafisha majitaka kwa asilimia 30 ifikapo 2020 kutoka kiwango cha asilimia 10 iliyopo sasa itakayogharimu Dola za Kimarekani Milioni 600 katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesema mfumo wa majitaka wa Jangwani utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kusafisha majitaka hayo mita za ujazo 200,000 kwa siku.

Mabomba yenye urefu wa kilomita 376 yatajengwa katika mradi utakaonzia kunazia Ubungo hadi Jangwani,Kinondoni, Mwananyamala, Msasani Katikati ya Jiji na Ilala.

Mhandisi Mwang’ingo amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha sehemu sehemu itakayoweza kusafisha mita za ujazo 25,000 kwa siku na mabomba yenye urefu wa kilomita 17.43 yatakayojengwa eneo la magomeni.

Aidha katika awamu ya kwanza,bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha kutumika na badala yake majitaka hayo yatakwenda kusafishiwa katika mtambo huo ambapo mtambo huu unajengwa kati ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Korea kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya Korea unaotarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 90 ambazo tayari zimepatikana.

No comments: