Kauli hiyo ya Ndugu Abdulrahman Kinana imekuja baada ya wananchi kuonyesha waziwazi kutokubali utendaji kazi wa mbunge huyo ambaye aliwekwa kitimoto na wananchi hao, wakisema amekuwa akipiga porojo tu badala ya kutatua matatizo yanayowakabili huku wakitolea mfano wa zahahati ya kata hiyo ambayo haina Jokofu la kuhifadhia dawa kwa zaidi ya miaka mitano sasa, jambo ambalo linawafanya akina mama wajawazito pamoja na wagonjwa wengine kupata adha kubwa kutokana na kukosa dawa katika zahanati hiyo, Wananchi hao wameongeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa mbunge huyo aliwaahidi kuleta mnara wa mawasiliano wa simu za mkononi kwa muda wa siku 100 jambo ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.Hata hivyo Katibu Mkuu Kinana ameahidi kuwanunulia jokofu hilo wananchi wa kata ya Loya ili kuondokana na adha hiyo (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UYUI-TABORA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi.



















No comments:
Post a Comment