Monday, May 05, 2014

Vigogo wa CCM Waung'uruma Kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar Nakusema Serikali Mbili Zatosha,Tatu Za Nini?

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .
 Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Ummy Mwalimu akionyesha ishara ya serikali mbili wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kibanda maiti na kuwataka wanawake wote wa Zanzibar kuungana katika kusimamia Muungano wa Tanzania.
 Mbili zatosha.
 Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
 Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
 Mama Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa Bunda Stephen Wassira akihutubia wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya Muungano kwanza kisha waje na hoja .
Mbunge wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC  Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .
Sehemu ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Picha na Adam Mzee
--
  • Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
  • Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
  • Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
  • Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .

No comments: