Monday, May 26, 2014

CCM WAFANYA MKUTANO MKUBWA SINGIDA, WAELEZEA MIPANGO YAKE YA MAENDELEO KWA WANANCHI

Mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo mkubwa ambao umerushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star Tv ni Dr. Charles Tizeba naibu waziri wa uchukuzi, Amos makala Naibu Waziri wa Maji, Mwigulu Nchemba naibu waziri wa Fedha na Uchumi na, Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Stephen Wasira Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Adam Malima Naibu waziri wa Fedha na Uchumi  na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mkoa wa Singida.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SINGIDA)3029Mwigulu Nchemba naibu waziri wa Fedha na Uchumi na, Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki na Naibu Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini Singida leo.28Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Singida27Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki Bw. Andrew Andalu akipongezwa na Mh. Stephen Wasira  mara baada ya  alipotangaza kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara mjini Singida, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida mjini Khamis Nguli na Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu wa CCM.26Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki Bw. Andrew Andalu akitoa ushuhuda uliomfanya aachane na CHADEMA na kujiunga na CCM.25Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makala akiwahutubia wananchi wakati akiwaelezea kuhusu mipango ya serikali kuhusu maji katika mkutano wa hadhara mjini Singida.24Naibu Waziri wa Uchukuizi Mh. Charles Tizeba akiwaelezea wananchi mipango ya serikali katika suala la ukarabati wa reli ya kati.23Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa meza kuu na viongozi mbalimbali katika mkiutano huo.22Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.21Baadhi ya wanachama wa CCM kutoka Isuna.20Mkuu wa mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone akiwaelezea wananchi mafanikio yaliyopatikana katika mkoa huo chini ya ilani ya uchaguzi ya CCM. 17Nyooomi33Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio katika mkutano huo.32Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai katikati na Nape Nnauye wakifurahia jambo katika mkutano huo.31Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohamed Dewji akizungumza na wananchi wa jimbo lake f15Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohamed Dewji wakiwa wamepanda bodaboda wakielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini Singida.16Msafara wa pikipiki ukielekea kwenye mkutano huo.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulhman Kinana akishiriki kazi ya useremala wakati alipotembelea mradi wa kikundi cha vijana seremala kinachoitwa Aikande Workshop mjini Singida.10Mitambo mipya ya maji katika mradi wa maji iliyofungwa katika kiiji cha Ng’aida manispaa ya Singida katika kupunguza tatizo la maji kwenye manispaa hiyo.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulhman Kinana akimsikiliza mhandisi wa maji wa SUWASA Mhandisi Isaack Nyakonji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo.8Mradi wenyewe12Mh. Mohammed Dewaji akishiriki katika kupiga ripu kwenye shule ya sekondari ya Mughanga  mjini Singida7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulhman Kinana akiondoka mara baada ya kukagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida, kulia ni Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki Mh. Mwigulu Nchemba na kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan na anayefuata ni mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji.6Pendael Masai Afisa Muuguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida  akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea hospitali hiyo kulia ni Mwigulu Nchemba Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi.5Baadhi ya majengo ya hospitali hiyo.1aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua  hospitali hiyo kutoka kulia ni Pendaeli Masai Afisa Mhuuguzi wa hospitali hiyo,  Mwigulu Nchemba Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi na kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan  na mkuuu wa mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wauguzi mbalimbali wa hospitali hiyo2aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Pendaeli Masai Afisa Mhuuguzi wa hospitali hiyo kulia nia Daktari Bingwa wa Afya ya Mama na mtoto katika hospitali hiyo Dr. Suleiman Mutani kushoto.1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Dr. Doroth Gwajima mganga mkuu wa mkoa wakati alipowasili katika hospitali hiyo.

No comments: