Rais Jakaya Kikwete Amfariji Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya Jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian anatarajiwa kuzikwa leo mchana(Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es Salaam .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU
Comments