RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jion, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa ya Balozi Sefue imeongeza kuwa uteuzi huu ulianza, Alhamisi, Mei 2014.
Comments