Wenyeviti wa Vyama Vya Upinzani Wawasili Zanzibar Tayari Kwa Mkutano wa Hadhara wa Pamoja Kuwashawishi Wananchi Kuukataa Mchakato wa Katiba Mpya
Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe Kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Kulia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI James Mbatia muda mfupi baada ya kuwasili zanzibar kwa ajili ya mkutano wa wa hadhara wa pamoja kuwashawishi wananchi kuukataa mchakato wa katiba leo
Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha kuwa wamepokea barua ya maombi hayo na tayari wameshawaruhusu, lakini kwa kufuata masharti yakiwamo kutotoa lugha za matusi katika majukwaa na kutoa kauli ambazo hazitahamasisha chuki.
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Habari na Haki za Binadamu wa CUF, Salum Bimani, alisema tayari maandalizi yameshakamilika na wameshapokea kibali cha kufanya mkutano huo kutoka kwa Jeshi la Polisi ukiwa na lengo la mshikamano wa vyama vya upinzani kuhusu muswaada wa rasimu ya katiba.
Alisema mkutano huo utahusisha chama cha CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi. Pia mkutano huo utahudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi na Bimani, mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti.

Comments