Friday, January 23, 2026

*MV NEW MWANZA YAZINDULIWA RASMI*








WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amezindua meli ya kisasa MV New Mwanza, akibainisha kuwa ni uwekezaji wa kimkakati wa Serikali katika kuimarisha usafiri wa majini, usalama wa abiria na kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa.

 “Serikali imejidhatiti kuhakikisha usafiri wa majini unakuwa salama, wa uhakika na unaowanufaisha wananchi,” — Dkt. Mwigulu Nchemba

MV New Mwanza ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400 na magari, huku safari ya Mwanza–Bukoba ikichukua takribani saa 6. Mradi huu umegharimu USD 51.83 milioni (takribani TSh bilioni 120.56).


 

No comments:

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...