Kigoma Yaitikia Wito wa ‘Kikwetu Kwetu’ OR Kigoma Answer The Calling ‘Kikwetu Kwetu’


 Msanii wa muziki nchini Lady Jaydee ‘Jide’ akitumbuiza kwenye tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wLake Tanganyika mjini Kigoma.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Izzo Bizness akiwapagawisha washabiki katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour Kigoma.
 Diamond akiongoza wasanii wenzake Mwasiti, Linex na Recho katika nyimbo ya ‘Leka Dutigite’ na kuwaamsha mashabiki waliofurika uwanja wa Lake Tanganyika katika tamasha la Kili Music Tour, mjini Kigoma.
 Umati wa mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour, wakifuatilia onyesho hilo lililofanyioka kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya yake katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika Kigoma.
Baadhi ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
---
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul, juzi  alifunika katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na umati wa mashabiki, Diamond alifanya onyesho la aina yake na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kupiga kelele.

Diamond ambaye alikuwa msanii wa mwisho kupanda kwenye jukwaa, aliwaita wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma kama Recho, Mwasiti pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Leka Dutigite na kuwaamsha mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.

Wasanii wengine ambao walitumbuiza katika onyesho hilo lenye ujumbe wa ‘Kikwetu Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Lady Jaydee, Barnaba, Ben Pol, Izzo Bizness, Recho, Prof. J, Fid. Q, Roma, Mwasiti, Linex pamoja na Kala Jeremiah.

Comments