Maelfu Wajitokeza Viwanja Vya Jangwani Jijini Dar es Salaam Mkutano wa Kudai Mchakato Huru wa Katiba Mpya

Umati wa watu waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kuwahamasisha wananchi kuungana na kudai mchakato huru wa katiba mpya unaoshirikisha wananchi wote uliofanyika Jumamosi kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azaveli Lwaitama.
 Askofu Zakaria Kakobe akihutubia katika Mkutano wa Katiba Viwanja vya Jangwani.
 Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akihutubia katika Mkutano wa Katiba Ulioitishwa na Umoja wa Vyama vya siasa, Wanaharakati na Viongozi wa Dini.
 Mnadhimu mkuu wa Kambi ya Upinzani na mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu akihutubia katika mkutano wa Katiba katika Viwanja vya Jangwani Dar es salaam.
 Mwanasheria wa Chadema Mh Mabere Marando akihutubia mamia ya wakazi wa Dar es salaam Katika Mkutano wa Katiba.
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia akihutubia wakazi wa Dar es salaam katika Mkutano wa suala la katiba uliofanyika katika viwanja vya Jangwani.
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano uliojumuisha Vyama vya Siasa, Wanaharakati na taasisi za Dini kujadili Suala la Mchakato wa Katiba unaoendelea.
 Wenyeviti wa vyama vya upinzani wakiwa wameshikina mikono kuonesha mshikamano wao wakati wa mkutano wa kuwahamasisha wananchi kuungana na kudai mchakato huru wa katiba mpya unaoshirikisha wananchi wote . Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa ADC, Lucas Limbu  Mwenyekiti wa NLD, Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa (UPDP), FahmiDovutwa. Picha Zote na Francis Dande
----
Vyama vya upinzani jana vilifanya mkutano mkubwa kuwashawishi wananchi kupinga kile walichokiita kuhujumiwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, wakitangaza Oktoba 10 kuwa siku ya Watanzania wote kushiriki katika maandamano kushinikiza wapewe haki ya kuandaa Katiba yao.

Wakizungumza kwa kupokezana katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam jana, wenyeviti wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, walieleza kuwa wataendelea kushirikisha taasisi za kiraia kupinga hujuma dhidi ya mchakato wa Katiba Mpya na kwamba hawatakubali endapo Rais Jakaya Kikwete atasaini Muswada wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea......

Comments