Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ajumuika na Wananchi katika Mazishi Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Meja Khatibu Shaaban Mshindo aliyefariki Dunia akiwa katika shughuli za ulinzi wa amani katika kikosi cha umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.
Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam.
WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa na mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuuteremsha katika ndege maalum ya Jeshi.
Wanajeshi wa JWTZ wakitembelea kwa mwendo wa pole wakiwa na Mwili wa Marehemu Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuwasili Zanzibar, tayari kwa mazishi yanayofanyika jioni hii katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba ya kuupokea Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja wa ndege wa Zanziba leo mchana na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika na Ndugu na Jamaa kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo.ulipowasili Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa mazishi jana jioni
Msafara wa Magari ya JWTZ ukiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea katika Msikiti wa Bezredi Muembeladu kwa kuusalia na maziko yatakayofanyika katika Kijiji chao Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja, saa kumi jioni.
Wapiganaji wa Jeshi la Wananachi wa Tanzania { JWTZ } wakitoa salamu zao za mwisho wakati wa mazishi ya kamanda wao Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani. Meja Khatib Shaaban ambae alikuwa Mkuu wa Kambi ya Kibaha alifariki dunia Mjini Goma Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa katika ulizi wa amani katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.
Mamia ya wananachi, ndugu na Jamaa walioshiriki kuusitiri mwili ma marehemu Meja Khatibu Shaaban katika mahali pake Huko Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongoza mamia ya wanajeshi, wananchi na Ndugu na jamaa katika Mazishi ya Meja wa Kikosi cha JWTZ Khatib Shaaban Mshindo, aliyeuawa Nchini DRC akiwa katika shughuli za ulinzi wa vikosivya Umoja wa Mtaifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed akitia udongo kwenye kaburi wakati wa mazinshi ya Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
Mwakilishi wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilivyopo Mjini Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Meja E.B. Samuel akitia udongo kuashiria ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika mazishi ya Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Kiongozi wa Familia ya Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo bwana Alhaji Machano Mtumweni mara baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kamanda huyo yaliyofanyika kijiji kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Comments