Thursday, September 05, 2013

Wabunge wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF watoka nje baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa

Wabunge wa Vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, na Chadema wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bungeni dodoma jana.Picha na Fidelis Felix  
---
 Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa.

Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini.
Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: “Kwendeni zenu, tumewazoea.”Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...