Tuesday, September 24, 2013

Mtanzania Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio la Kenya aelezea yaliyomkuta, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba asema Tumejipanga

 Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio la Kenya akiwa hospitali
---
Wakati wa Jeshi la Polisi la Tanzania likisema linafuatilia taarifa za vitisho za kundi la Al-Shabaab la Somalia za kushambulia, Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio la Kenya ameelezea yaliyomkuta.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema jana kuwa wameanza kufuatilia kwa undani taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la Al-Shabaab linajipanga kuishambulia Tanzania na Uganda.

DCI Manumba alikiri kusikia taarifa hizo na kusema kuwa Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina: “Siwezi kukueleza ni uchunguzi wa aina gani tutakaofanya, hiyo ni siri yetu.”

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Eric Komba alisema kuwa kuna uwezekano taarifa hizo zikapikwa na wajanja wachache kwa ajili ya kuwajengea hofu wananchi.Kwa habari zaidibofya na Endelea.......

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...