AAR YATOA HUDUMA YA AFYA KWA WASHIRIKI WA BSS 2013

 Dactari  Richard kutoka  AAR akitoa kipimo cha   BMI kwa mmoja ya washiriki wa BSS 2013 kambini mbezi Dar-es-salaam.
Mshiriki wa BSS  Elizabeth Mwakijambile  akiongea na waandishi wa habari baada ya kupata vipimo vya afya kutoka AAR walipoenda kutembelewa kambini kwao Mbezi.
 Muuguzi Salome Mkilima kutoka  AAR  akimpima  BP mshiriki wa BSS 2013 kambini Mbezi Beach Dar-es-salaam.
Washiriki wa  Bongo Star Search  wakipata vipimo vya BMI na BP kabla ya kupanda jukwaani.
 Dr. Bamuhimbisa Richard kutoka AAR Healthcare akitoa mafunzo kwa washiriki wa BSS 2013 ya jinsi ya kuishi maisha bora kwa kuwa waangalifu na afya zao,walipokua kwenye kambi yao Mbezi Beach.
 Afisa Mahusiano wa AAR HealthCare  Amisa Juma  akiwapa mafunzo washiriki wa BSS 2013   kuhusu afya zao ,kuchoto ni Bi, Fatma Omary, Maina Thadei na Amina Chibaba.
AAR Healthcare wakiwa na washiriki wa  BSS 2013.
----  
Hivi karibuni AAR Healthcare imefanya  vipimo vya afya kwa washiriki wa Bongo Star Search  mwaka 2013, vipimo hivyo vikiwamo BMI, BP  pamoja na kipimo cha kisukari 

Washiriki hao ambao kwa sasa wamebaki  15 ,walipewa  pia mafunzo ya kiafya kutoka  kwa  Madactari wa AAR  ya jinsi ya kuishi maisha yao kwa afya njema.

“Dhumuni la kuwafanyia  washiriki vipimo vya  afya, ni wao wenyewe kuweza  kutambua  afya  zao  kabla ya kuanza kupanda  jukwaani, kupata ushauri  wa jinsi ya kutunza afya zao kwa kipindi chote cha mashindano na hata baada ya mashindano” . Alisema Afisa Mahusiano wa AAR Amisa Juma.

Bi. Juma alimalizia kwa kusema “ Sisi kama wadau  wakubwa katika afya nchini, tumegundua  vijana  ndo  waathirika wakubwa wa afya, kwaiyo  tumeamua kutumia jukwaa hili la BSS  kuweza kusaidia na kutoa mchango mkubwa kwa washiriki na jamii kwa ujumla” .

Hii ni mara ya pili kwa AAR kudhamini mashindano haya ya BSS, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2011.

Comments