WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA

  Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine aliyoambatana nao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,  leo ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya,  kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba 2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na Hospitali ya MP Shah.Picha Kwa hisani ya Issa Michuzi 

Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Comments